Al-Hashr 59:23
الحشرهُوَ ٱللَّهُ ٱلَّذِى لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلْمَلِكُ ٱلْقُدُّوسُ ٱلسَّلَـٰمُ ٱلْمُؤْمِنُ ٱلْمُهَيْمِنُ ٱلْعَزِيزُ ٱلْجَبَّارُ ٱلْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ
Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipokuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, anayefanya analolitaka, Mkubwa. Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayomshirikisha nayo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu, Anaye fanya analo litaka, Mkubwa, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo mshirikisha nayo. [23]
[23] Yeye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye, Mwenye kumiliki kila kitu kwa hakika, Aliye safika na kila upungufu, Aliye takasika na kila lisio mwelekea, Mwenye kusalimika na yote ya upungufu, Mwenye kuwaamini na kuwasadiki Mitume wake aliyo wapa nguvu kwa miujiza, Mlinzi Mwenye kuangalia kila kitu, Mwenye kushinda basi hashindwi na chochote, Mkubwa wa shani katika nguvu na utawala, Mwenye kutukuka na kila kisicho kuwa laiki na uzuri wake na utukufu wake, Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo wanayo mshirikisha nayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yeye Ndiye Allah Mtukufu Mwenye kuabudiwa kwa haki, Ambaye hakuna Mola isipokuwa Yeye, Mmiliki wa vitu vyote, Anayeviendesha bila kizuizi chochote wala upinzani, Aliyetakasika na kila upungufu, Aliyeepukana na kila aibu, Anayewasadikisha Mitume Wake na Manabii kwa dalili zilizo wazi Alizowatuma nazo, Anayewatunza viumbe Wake katika matendo yao, Aliye Mshindi Ambaye hakuna wa kushindana naye, Aliye Jabbari Ambaye Amewatendesha nguvu waja wote, na Ambaye viumbe vyote vimemdhalilikia, Aliye Mkubwa Mwenye kiburi na utukufu. Ametakasika Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na kila kile ambacho wanamshirikisha nacho katika kumuabudu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net