Al-Mujaadila 58:22
المجادلةلَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ يُوَآدُّونَ مَنْ حَآدَّ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَلَوْ كَانُوٓا۟ ءَابَآءَهُمْ أَوْ أَبْنَآءَهُمْ أَوْ إِخْوَٰنَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ كَتَبَ فِى قُلُوبِهِمُ ٱلْإِيمَـٰنَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ ۖ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَا ۚ رَضِىَ ٱللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا۟ عَنْهُ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ حِزْبُ ٱللَّهِ ۚ أَلَآ إِنَّ حِزْبَ ٱللَّهِ هُمُ ٱلْمُفْلِحُونَ
Huwakuti watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao ameandika katika nyoyo zao Imani, na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake. Na atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Humo watakaa daima. Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na wao wawe radhi naye. Hao ndio Hizbullahi (Kundi la Mwenyezi Mungu). Hakika Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufanikiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Huwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao ameandika katika nyoyo zao Imani, na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake. Na atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Humo watakaa daima. Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na wao wawe radhi naye. Hao ndio Hizbullahi, Kundi la Mwenyezi Mungu. Hakika Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufanikiwa. [22]
[22] Huwakuti watu wanao msadiki Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho wanapendana na wenye kumfanyia uadui Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au ni watoto wao, au ni ndugu zao, au ni jamaa zao. Hao ambao hawafanyi urafiki na wanao mpinga Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu ameithibitisha Imani katika nyoyo zao, na amewaunga mkono kwa nguvu zinazo tokana naye Yeye Mwenyewe, na atawatia katika Mabustani yapitayo mito kati yake wakikaa humo milele. Neema zake haziwakatikii. Mwenyezi Mungu amewapenda hao, na wao wamempenda. Hao ndio wanao ambiwa kuwa ni katika Hizbullahi, yaani Kundi la Mwenyezi Mungu. Hakika ni kweli Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufuzu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hutakuta, (ewe Mtume), watu wanaomuamini Allah Mtukufu na Siku ya Mwisho na wanaofanya matendo waliyoamrishwa na Allah Mtukufu, wakiwapenda na kuwategemea wale wanaomfanyia uadui Allah Mtukufu na Mtume Wake na wanaoenda kinyume na amri zao, hata kama ni baba zao au watoto wao au ndugu zo au jamaa zao wa karibu. Hao wanaofanya urafiki kwa ajili ya Allah Mtukufu na wanaochukia na kufanya uadui kwa ajili ya kunusuru dini yake ndio ambao Allah Mtukufu Ameithibitisha Imani ndani ya nyoyo zao, na Akawatia nguvu kwa kuwapa ushindi utokao Kwake, na msaada dhidi ya adui yao duniani, na Atawaingiza huko Akhera kwenye mabustani ya Peponi ambayo chini ya miti yake inapita mito, hali ya kukaa humo milele, Amewapa radhi Zake na hatawakasirikia, na wao wameridhika na Mola wao kwa yale Aliyowapatia ya utukufu na daraja kubwa. Hao ndio kundi la Allah Mtukufu na walioshikamana naye, na hao ndio wenye kufaulu kwa kupata furaha ya duniani na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net