Al-Mujaadila 58:16
المجادلةٱتَّخَذُوٓا۟ أَيْمَـٰنَهُمْ جُنَّةً فَصَدُّوا۟ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ فَلَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ
Wamefanya viapo vyao ni ngao, na wakaizuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi hao watapata adhabu ya kufedhehesha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wamefanya viapo vyao ni ngao, na wakaipinga Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi hao watapata adhabu ya kufedhehesha. [16]
[16] Wamefanya viapo vyao kuwa ndio viwe ni kinga ya kuwakinga wasiuliwe wenyewe, na watoto wao wasiwe mateka, na mali yao yasiwe ngawira. Kwa hayo wakaizuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watapata adhabu ya fedheha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanafiki wamevifanya vile viapo vyao vya urongo ni kinga yao wasipate kuuawa kwa ukafiri wao na kuwazuia Waislamu wasiwapige vita na kuchukua mali yao. Na kwa ajili hiyo wanajizuia wao na kuwazuia wengine na njia ya Allah Mtukufu, nayo ni Uislamu. Basi watapata adhabu yenye kudhalilisha Motoni, kwa kufanya kiburi kwao na kujiepusha kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, na kwa kuzuia kwao njia Yake isifuatwe.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net