Al-Hadid 57:9
الحديدهُوَ ٱلَّذِى يُنَزِّلُ عَلَىٰ عَبْدِهِۦٓ ءَايَـٰتٍۭ بَيِّنَـٰتٍ لِّيُخْرِجَكُم مِّنَ ٱلظُّلُمَـٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ ۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ بِكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ
Yeye ndiye anayemteremshia mja wake Aya zinazobainisha wazi ili akutoeni gizani hadi kwenye nuru. Na hakika Mwenyezi Mungu kwenu ni Mpole mno, Mwingi wa kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yeye ndiye anaye mteremshia mja wake Aya zinazo bainisha wazi ili akutoeni gizani muingie kwenye nuru. Na hakika Mwenyezi Mungu kwenu ni Mpole, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yeye Ndiye Anayemteremshia mja Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), aya za Qur’ani zilizofafanuliwa, zilizo wazi, ili Awatoe kwenye giza la ukafiri na kuwatia kwenye mwangaza wa Imani. Na hakika Allah Mtukufu, kwa kule kuwatoa nyinyi kwenye giza na kuwatia kwenye mwangaza, Anawarehemu rehema kunjufu katika maisha yenu ya sasa ya ulimwenguni na maisha yenu ya baadaye, na awalipe malipo mazuri kabisa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net