Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 57 · Aya ya 27

Al-Hadid 57:27

الحديد

ثُمَّ قَفَّيْنَا عَلَىٰٓ ءَاثَـٰرِهِم بِرُسُلِنَا وَقَفَّيْنَا بِعِيسَى ٱبْنِ مَرْيَمَ وَءَاتَيْنَـٰهُ ٱلْإِنجِيلَ وَجَعَلْنَا فِى قُلُوبِ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُ رَأْفَةً وَرَحْمَةً وَرَهْبَانِيَّةً ٱبْتَدَعُوهَا مَا كَتَبْنَـٰهَا عَلَيْهِمْ إِلَّا ٱبْتِغَآءَ رِضْوَٰنِ ٱللَّهِ فَمَا رَعَوْهَا حَقَّ رِعَايَتِهَا ۖ فَـَٔاتَيْنَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنْهُمْ أَجْرَهُمْ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَـٰسِقُونَ

Maana

Tena tukafuatisha nyuma yao Mitume wengine, na tukamfuatisha Isa mwana wa Mariamu, na tukampa Injili. Na tukaweka katika nyoyo za wale waliomfuata upole na rehema. Na umonaki (utawa wa mapadri) wameuzua wao. Sisi hatukuwaandikia hayo, ila kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Lakini hawakuufuata inavyotakiwa kuufuata. Basi wale walioamini katika wao tuliwapa ujira wao. Na wengi wao ni wavukao mipaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Tena tukafuatisha nyuma yao Mitume wengine, na tukamfuatisha Isa bin Mariamu, na tukampa Injili. Na tukajaalia katika nyoyo za walio mfuata upole na rehema. Na umonaki (utawa wa mapadri) wameuzua wao. Sisi hatukuwaandikia hayo, ila kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Lakini hawakuufuata inavyo takiwa kuufuata. Basi wale walio amini katika wao tuliwapa ujira wao. Na wengi wao ni wapotovu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukafuatisha, kwenye kizazi cha Nûḥ na Ibrãhîm, (Mitume wetu) tuliowatuma kwa hoja zilizo wazi, na tukamfuatisha ‛Ῐsā mwana wa Maryam na tukampa Injili, na tukajaalia ndani ya nyoyo za wale waliomfuata na kuwa kwenye dini yake ulaini na huruma, wakawa wanapendana wao kwa wao. Na kisha hao wafuasi walizusha taratibu za kuabudu, kwa kuvuka mpaka katika ibada, ambazo hatukuwaamrisha nazo isipokuwa ni wao wenyewe waliojilazimisha nazo kwa lengo la kupata radhi za Allah Mtukufu, lakini hawakusimama nazo vile inavyotakiwa kusimama kwa kutovuka mpaka. Basi tukawapa wale walioamini miongoni mwao malipo yao kulingana na Imani yao, na wengi miongoni mwao ni wenye kutoka nje ya utiifu wa Allah Mtukufu, na ni wenye kumkanusha Nabii Wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hadid

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net