Al-Hadid 57:24
الحديدٱلَّذِينَ يَبْخَلُونَ وَيَأْمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلْبُخْلِ ۗ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْغَنِىُّ ٱلْحَمِيدُ
Ambao wanafanya ubahili, na wanaamrisha watu wafanye ubahili. Na anayegeuka, basi Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha, Msifiwa mno.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ambao wanafanya ubakhili, na wanaamrisha watu wafanye ubakhili. Na anaye geuka, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Msifiwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawa wenye kujiona ndio wale wanaoifanyia ubahili mali yao, wasiitoe katika njia ya Allah Mtukufu, na wakawaamuru watu wawe mabahili kwa kuwapambia huo ubahili. Na yoyote anayezunguka nyuma kwa kuacha kumtii Allah Mtukufu hamdhuru yoyote isipokuwa nafsi yake, na hatamdhuru Allah Mtukufu chochote, kwani Allah Mtukufu Ndiye Mkwasi Asiyehitajia viumbe vyake, Mwenye kuhimidiwa Ambaye Ana kila sifa njema iliyokamilika, na kila tendo zuri ambalo Anastahiki kushukuriwa kwalo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net