Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 57 · Aya ya 17

Al-Hadid 57:17

الحديد

ٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ يُحْىِ ٱلْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ ٱلْـَٔايَـٰتِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ

Maana

Jueni kwamba Mwenyezi Mungu huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Hakika tumekubainishieni Ishara ili mpate kuzingatia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Jueni kwamba Mwenyezi Mungu huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Tumekubainishieni Ishara ili mpate kuzingatia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Jueni kwamba Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, Anaihuisha ardhi kwa mvua baada ya kufa kwake ikatoa mimea. Basi vilevile Allah Mtukufu ni Muweza wa kuhuisha wafu Siku ya Kiyama, na Ndiye Muweza wa kuzilainisha nyoyo baada ya kususuwaa kwake. Kwa hakika tumewafafanulia dalili za uwezo wetu, ili mpate kuzielewa na kuwaidhika.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hadid

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net