Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 57 · Aya ya 14

Al-Hadid 57:14

الحديد

يُنَادُونَهُمْ أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ ۖ قَالُوا۟ بَلَىٰ وَلَـٰكِنَّكُمْ فَتَنتُمْ أَنفُسَكُمْ وَتَرَبَّصْتُمْ وَٱرْتَبْتُمْ وَغَرَّتْكُمُ ٱلْأَمَانِىُّ حَتَّىٰ جَآءَ أَمْرُ ٱللَّهِ وَغَرَّكُم بِٱللَّهِ ٱلْغَرُورُ

Maana

Watawaita wawaambie: 'Kwani hatukuwa pamoja nanyi?' Watawaambia: 'Ndiyo, lakini mlijifitini wenyewe, na mkatazamia mabaya (Waumini), na mkatia shaka, na matamanio ya nafsi zenu yakakudanganyeni mpaka ilipokuja amri ya Mwenyezi Mungu, na mdanganyifu yule[1] akakudanganyeni msimfuate Mwenyezi Mungu.

[1] Yaani Shetani.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watawaita wawaambie: Kwani vile hatukuwa pamoja nanyi? Watawaambia: Ndiyo, lakini mlijifitini wenyewe, na mkasitasita, na mkatia shaka, na matamanio ya nafsi zenu yakakudanganyeni. mpaka ilipo kuja amri ya Mwenyezi Mungu, na mdanganyifu akakudanganyeni msimfuate Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hapo wale wanafiki wawaite Waumini kwa kusema, «Kwani hatukuwa na nyinyi duniani tukitekeleza ibada za Dini kama nyinyi?» Na Waumini wawaambie, Ndio, mlikuwa na sisi kidhahiri, lakini nyinyi mlijiangamiza wenyewe kwa unafiki na kufanya maasia, na mkingojea kwa hamu Nabii afe na Waumini wapatwe na mikasa, mkakufanyia shaka kule kufufuliwa baada ya kufa, na yakawadanganya nyinyi matumaini yenu ya urongo na mkasalia katika hali hiyo mpaka mauti yakawajia. Na Shetani aliwadanganya nyinyi kuhusu Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hadid

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net