Ar-Rahmaan 55:13
الرحمنفَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayoikanusha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Bas ni neema gani za Mola wenu, za kidini na za kidunia, «enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha»? Na ni jawabu nzuri lililoje la majini alipowasomea Nabii, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), sura hii, kila akisoma kwenye aya hii walikuwa wakisema, «Hakuna chochote miongoni mwa neema zako, ewe Mola wetu, tunachokanusha. Sifa njema zote ni zako.» Na hivi ndivyo inavyotakiwa kwa mja anapoelezewa neema za Allah Mtukufu na mema Yake akubali na amshukuru Allah Mtukufu kwa neema hizo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net