Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 54 · Aya ya 40

Al-Qamar 54:40

القمر

وَلَقَدْ يَسَّرْنَا ٱلْقُرْءَانَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ

Maana

Na hakika tumeisahilisha Qur-ani kuikumbuka. Lakini yupo anayekumbuka?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika tumeisahilisha Qur'ani kuikumbuka. Lakini yupo anaye kumbuka? [40]

[40] Na hakika tumeifanya Qur'ani ni sahali kwa ajili ya mawaidha na mazingatio. Je! Yupo anaye waidhika?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kwa hakika tumeyawepesisha matamko ya Qur’ani, ili isomwe na ihifadhiwe, na tumeiwepesisha maana yake, ili ifahamike na izingatiwe kwa anayetaka kuwaidhika na kuzingatia. Basi je kuna mwenye kuwaidhika nayo?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qamar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net