Al-Qamar 54:37
القمروَلَقَدْ رَٰوَدُوهُ عَن ضَيْفِهِۦ فَطَمَسْنَآ أَعْيُنَهُمْ فَذُوقُوا۟ عَذَابِى وَنُذُرِ
Na walimtaka awape wageni wake. Tukayapofua macho yao, na tukawaambia: 'Onjeni basi adhabu na maonyo yangu!'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walimtaka awape wageni wake. Tukayapofua macho yao, na tukawaambia: Onjeni basi adhabu na maonyo yangu! [37]
[37] Wakamtaka awape wageni wake wawatende fiili yao, tukayafuta macho yao kuwa ni malipo kwa hilo walilo litaka. Basi waambie kwa kuwakejeli: Igugumieni adhabu yangu, na maonyo yangu!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa hakika walitaka ruhusa yake kufanya uchafu na wageni wake ambao ni Malaika, tukayafuta macho yao wasione chochote na wakaambiwa, «Onjeni adhabu yangu na onyo langu alilowaonya nalo Lûṭ, amani imshukie».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net