Al-Qamar 54:35
القمرنِّعْمَةً مِّنْ عِندِنَا ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِى مَن شَكَرَ
Kwa neema inayotoka kwetu. Hivyo ndivyo tumlipavyo anayeshukuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa neema inayo toka kwetu. Hivyo ndivyo tumlipavyo anaye shukuru. [35]
[35] Kwa kuwapa neema iliyo toka kwetu. Neema kama hizo kubwa kubwa ndivyo tunavyo walipa wenye kuishukuru neema yetu kwa imani yao na ut'iifu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ikiwa ni neema itokayo kwetu juu yao. Kama tulivyompa malipo mema Lûṭ na watu wake wa nyumbani, tukawapa neema na tukawaokoa na adhabu yetu, ndivyo tunavyowalipa mema waliotuamini na kutushukuru.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net