Al-Qamar 54:31
القمرإِنَّآ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ صَيْحَةً وَٰحِدَةً فَكَانُوا۟ كَهَشِيمِ ٱلْمُحْتَظِرِ
Hakika Sisi tuliwatumia ukelele mmoja tu, wakawa kama mabuwa ya kujengea ua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Sisi tuliwapelekea ukelele mmoja tu, wakawa kama mabuwa ya kujengea uwa. [31]
[31] Sisi tuliwapatiliza kwa ukelele mmoja tu, wakawa kama miti mikavu anayo ikusanya yeyote atakaye kujengea boma la uwa wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sisi tuliwateremshia Jibrili, akawapigia ukelele mmoja, wakaangamia hadi wa mwisho wao, wakawa ni kama nyasi zilizokauka zilizo nyepesi kuvunjika, zinazofanyiwa boma la ngamia na mifugo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net