Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 54 · Aya ya 17

Al-Qamar 54:17

القمر

وَلَقَدْ يَسَّرْنَا ٱلْقُرْءَانَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ

Maana

Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur-ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anayekumbuka?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka? [17]

[17] Ninaapa, tumeifanya Qur'ani iwe sahali kukumbukwa na kutoa mawaidha. Lakini je, yupo wa kuwaidhika?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika tumeyawepesisha matamko ya Qur’ani ili isomwe na ihifadhiwe, na pia maana yake ili ieleweke na izingatiwe. Je kuna mwenye kuwaidhika nayo? Katika aya hii na mfano wake katika hii Sura kuna kuhimiza kusoma Qur’ani kwa wingi, kujifunza na kuifundisha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qamar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net