Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 54 · Aya ya 12

Al-Qamar 54:12

القمر

وَفَجَّرْنَا ٱلْأَرْضَ عُيُونًا فَٱلْتَقَى ٱلْمَآءُ عَلَىٰٓ أَمْرٍ قَدْ قُدِرَ

Maana

Na tukazipasua ardhi kwa chemichemi, yakakutana maji kwa jambo lililokwisha pangwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tukazipasua ardhi kwa chemchem, yakakutana maji kwa jambo lilio kadiriwa. [12]

[12] Na tukaipasua ardhi kwa chemchem zikitibuka maji. Yakakutana maji ya mbinguni na maji ya ardhi kuwahiliki, kama alivyo kadiria Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tukapasua ardhi tukatoa chemchemi za maji yanayotoka kwa kasi, yakakutana maji ya mbinguni na maji ya ardhini kuwaangamiza wao kwa vile Alivyowakadiria Allah Mtukufu, yakiwa ni malipo ya ushirikina wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qamar

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net