Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 53 · Aya ya 46

An-Najm 53:46

النجم

مِن نُّطْفَةٍ إِذَا تُمْنَىٰ

Maana

Kutokana na mbegu ya uzazi inapomiminwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa. [46]

[46] Kutokana na manii yanayo miminwa. Makusudio ya Aya hii tukufu ni kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba Yeye ameumba waume na wake katika wanaadamu na wanyama wote kutokana na tone ya manii ambayo humo humo mna ume na uke. Na juu ya udogo wake na udhaifu wake ndio chemchem ya uhai. Umuujiza wa Qur'ani unadhihirika katika Aya hii tukufu ukikumbuka kuwa ulimwengu ulikuwa haujui mpaka hivi karibu kuwa katika maji ya mwanamume ndio zimo mbegu "sperms" na katika maji ya mwanamke mna vijiyai "ova", ndio vikikutana vijidudu vya manii ya mwanamume na vijiyai vya mwanamke vikawa kitu kimoja ndio hiyo huwa mimba. Ukweli huu ulitajwa na Qur'ani kabla ya kuvumbuliwa na ilimu za Sayansi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kutokana na tone la manii linalomiminwa kwenye kizazi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Najm

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net