An-Najm 53:35
النجمأَعِندَهُۥ عِلْمُ ٱلْغَيْبِ فَهُوَ يَرَىٰٓ
Je, anayo huyo elimu ya ghaibu, basi ndiyo anaona?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Anayo huyo ilimu ya ghaibu, basi ndio anaona? [35]
[35] Je! Huyo anayo ilimu ya kujua mambo ya ghaibu, basi kwa hivyo ndio anayajua yanayo mpelekea kuiacha kuifuata Haki, na akafanya ubakhili wa mali?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je huyu anayekata kheri yake ya kutoa ana ujuzi wa ghaibu kuwa itamuishia mali yake ndipo akaizuia asiitoe, na akawa analiona hilo waziwazi? Mambo si hivyo! Hakika ni kwamba yeye aliacha kutoa sadaka na kufanya kheri, kutenda wema na kuunga udugu kwa ubahili na uchoyo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net