An-Najm 53:2
النجممَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَىٰ
Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea. [2]
[2] ya kwamba Muhammad hakuiacha Njia iliyo sawa ya kufuata Haki, na wala hakupata kuitakidi upotovu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
(kwamba Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), hakupotoka kwenye njia ya uongofu na haki, na hakutoka nje ya njia ya usawa. Bali yeye yuko kwenye upeo wa unyoofu, usawa na uthabiti.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net