Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 53 · Aya ya 18

An-Najm 53:18

النجم

لَقَدْ رَأَىٰ مِنْ ءَايَـٰتِ رَبِّهِ ٱلْكُبْرَىٰٓ

Maana

Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi. [18]

[18] Hakika ameona mengi katika Ishara za Mwenyezi Mungu na maajabu yake makubwa makubwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), aliona, usiku wa Mi‛rāj (kwenda mbinguni) alama kubwa zinazojulisha uwezo wa Allah Mtukufu na ukubwa Wake miongoni mwa Pepo, Moto na vinginevyo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Najm

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net