Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 52 · Aya ya 49

At-Tur 52:49

الطور

وَمِنَ ٱلَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَإِدْبَـٰرَ ٱلنُّجُومِ

Maana

Na usiku pia mtakase, na zinapokuchwa nyota.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na usiku pia mtakase, na zinapo kuchwa nyota. [49]

[49] Na tafuta usiku usiku nafasi ya kumsabihi, yaani kumtakasa, Mwenyezi Mungu, na mtakase pia wakati zinapo kuchwa nyota, yaani alfajiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kwenye kipindi cha usiku mtakase Mola wako kwa kumsifu, umtukuze na uswali kwa ajili yake. Na ufanye hayo kwenye kipindi cha Swala ya Asubuhi wakati wa nyota kuondoka. Katika aya hizi pana kuthibitisha sifa ya macho mawili kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kama inavyonasibiana na Yeye, bila kufananisha na viumbe Vyake au kuieleza dhati Yake vile ilivyo, kutakasika na kila sifa ya upungufu ni Kwake na sifa njema zote ni Zake, kama lilivyothibiti hilo katika Sunnah na kukubaliana juu yake wanavyuoni waliopita wa Ummah huu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tur

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net