Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 52 · Aya ya 35

At-Tur 52:35

الطور

أَمْ خُلِقُوا۟ مِنْ غَيْرِ شَىْءٍ أَمْ هُمُ ٱلْخَـٰلِقُونَ

Maana

Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? [35]

[35] Kwani wao wameumbwa bila ya kuweko Muumbaji, au wao wamejiumba wenyewe, basi kwa hivyo ati ndio hawamtambui Muumbaji wa kumuabudu?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, wameumbwa hawa washirikina bila kuwako mwenye kuwaumba au wamejiumba wenyewe? Na yote mambo mawili haya yametenguka na hayawezekani. Na kwa hivyo, inalazimika kuwa Allah Mtukufu Ndiye Aliyewaumba, na Yeye Peke Yake Ndiye Ambaye hakuna anayepasa kuabudiwa, wala kufaa kuabudiwa kwa haki, isipokuwa Yeye.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tur

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net