At-Tur 52:32
الطورأَمْ تَأْمُرُهُمْ أَحْلَـٰمُهُم بِهَـٰذَآ ۚ أَمْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ
Au hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Au hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu? [32]
[32] Bali ndio akili zao zinawaamrisha waseme maneno hayo yanayo gongana. Kwani kohani na mtunga mashairi ni watu wenye fahamu na akili; na mwendawazimu hana akili. Lakini hawa ni watu walio pita mipaka katika inadi zao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Au zinawaamuru akili zao, (hao wakanushaji), ziseme neno hili linalogongana? kwani uhakika ni kuwa sifa ya ukuhani, na utungaji mashairi, na wendawazimu haiwezekani kukutana wakati mmoja Bali wao ni watu waliovuka mipaka katika uasi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net