Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 52 · Aya ya 23

At-Tur 52:23

الطور

يَتَنَـٰزَعُونَ فِيهَا كَأْسًا لَّا لَغْوٌ فِيهَا وَلَا تَأْثِيمٌ

Maana

Watapeana humo bilauri zisizo na vinywaji vya kuleta maneno ya upuuzi wala dhambi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watapeana humo bilauri zisio na vinywaji vya kuleta maneno ya upuuzi wala dhambi. [23]

[23] Huko Peponi watakuwa wakipeana kwa mapenzi bilauri zilio jaa vinywaji visio leta maneno yasiyo na maana wala vitendo vya dhambi, yaani havilevi na kuondoa akili.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na miongoni mwa starehe hizo ni kuwa watapeana gilasi za pombe, (mmoja wao atampa mwenzake), ili furaha yao ikamilike. Kinywaji hiki kinatafautiana na pombe ya duniani, hakimleweshi akili mwenye kukinywa, wala hakisababishi kufanya vitendo vya asiyekuwa na Akili, wala maneno ya makosa na maasia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tur

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net