Adh-Dhaariyat 51:55
الذارياتوَذَكِّرْ فَإِنَّ ٱلذِّكْرَىٰ تَنفَعُ ٱلْمُؤْمِنِينَ
Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini. [55]
[55] Wewe dumisha kukumbusha, kwani ukumbusho huwazidisha Waumini kufumbua macho na kuwa na nguvu za yakini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Pamoja na kuwapuuza wao, (ewe Mtume), na kutoshughulika na ufedhuli wao, endelea kuwakumbusha wale uliotumwa kwao, kwani ukumbusho wananufaika nao wale wenye nyoyo zenye kuamini, na katika kufanya mawili hayo kuna kusimamisha hoja kwa wenye kuipa mgongo haki.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net