Adh-Dhaariyat 51:37
الذارياتوَتَرَكْنَا فِيهَآ ءَايَةً لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ ٱلْعَذَابَ ٱلْأَلِيمَ
Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanaoiogopa adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanao iogopa adhabu chungu. [37]
[37] Na katika mji huo tumeacha alama ya maangamizo ya watu wake, ili wapate kuzingatia wanayo ikhofu adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tukaacha kwenye mji huo uliotajwa mabaki ya adhabu iwe ni alama ya uwezo wa Allah Mtukufu Aliyetukuka na vile alivyowatesa makafiri. Ili iwe ni zingatio kwa wale wanaoiogopa adhabu ya Allah Mtukufu iliyo kali na yenye kuumiza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net