Adh-Dhaariyat 51:15
الذارياتإِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى جَنَّـٰتٍ وَعُيُونٍ
Hakika wacha Mungu watakuwa katika Mabustani ya mbinguni na chemchemi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem. [15]
[15] Hakika walio mt'ii Mwenyezi Mungu na wakamkhofu watakuwa wananeemeka katika Mabustani na chemchem za Peponi ambazo haziwezi kusifika hakika yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale wanaomcha Allah Mtukufu watakuwa kwenye mabustani ya Pepo makubwa na chemchemi za maji yenye kutembea. Allah Mtukufu Atawapa yote wanayoyatamani ya aina mbalimbali za starehe.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net