Adh-Dhaariyat 51:12
الذارياتيَسْـَٔلُونَ أَيَّانَ يَوْمُ ٱلدِّينِ
Wanauliza: 'Ni lini hiyo siku ya malipo?'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo? [12]
[12] Wanauliza kwa kejeli, kwa kuwa wanaona hayawi hayo: Lini itakuwa hiyo siku ya malipo?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanauliza hawa wenye kukanusha suali la kuonyesha kuwa ni jambo lisilowezekana na la kuonyesha ukanushaji, «Ni lini Siku ya kuhesabiwa na kulipwa?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net