Qaaf 50:8
قتَبْصِرَةً وَذِكْرَىٰ لِكُلِّ عَبْدٍ مُّنِيبٍ
Yawe haya ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kurejea (kwa Mwenyezi Mungu).
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yawe haya ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kuelekea. [8]
[8] Tumejaalia hayo aone na akumbuke kila mja mwenye kurejea kwa Mola wake Mlezi, akafikiri Ishara za uwezo wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Ameumba mbingu, ardhi na vilivyomo baina ya hivyo viwili miongoni mwa alama kubwa, ili viwe ni mazingatio ya kumfanya mtu aone na atoke kwenye giza la ujinga, na ni ukumbusho kwa kila mja mnyenyekevu, mwenye kuogopa, na mwenye kurejea kwa Allah Mtukufu Aliyeshinda na kutukuka.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net