Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 50 · Aya ya 6

Qaaf 50:6

ق

أَفَلَمْ يَنظُرُوٓا۟ إِلَى ٱلسَّمَآءِ فَوْقَهُمْ كَيْفَ بَنَيْنَـٰهَا وَزَيَّنَّـٰهَا وَمَا لَهَا مِن فُرُوجٍ

Maana

Je, hawaangalii mbingu zilizo juu yao! Vipi tulivyozijenga, na tukazipamba. Wala hazina nyufa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Hawaangalii mbingu zilizo juu yao! Vipi tulivyo zijenga, na tukazipamba. Wala hazina nyufa. [6]

[6] Wameghafilika hata hawaitazami mbingu ilivyo nyanyuliwa juu yao bila ya nguzo? Vipi tumetengeneza ujenzi wake, na tukaipamba kwa nyota, na haina nyufa za kuitia kombo! Mbingu ni kote kulio juu yetu, na ndani yake vimo vitu vya namna mbali mbali, vinaogelea katika njia zao, nyota na sayari. Na hayo ni kwa nidhamu ya uangalizi mkubwa, na mshikamano ulio timia, na vilevile zinafuata kwa mpango wake kuwafikiana na kanuni za mvutano, basi hazitelezi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani walighafilika walipokanusha Ufufuzi, wasiangalie mbingu juu yao: vipi tulizijenga zikiwa zimelingana sawa pande zote, limeimarika umbile lake, na tukazipamba kwa nyota, na hazina mipasuko na nyufa, zimesalimika na hitilafu na kasoro?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Qaaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net