Qaaf 50:38
قوَلَقَدْ خَلَقْنَا ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِى سِتَّةِ أَيَّامٍ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٍ
Na bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita; na wala hayakutugusa machovu yoyote.[1]
[1] Aya hii ilishuka ili kuwapinga Mayahudi na Wakristo wanaodai kwamba Mwenyezi Mungu alipumzika katika siku ya saba baada ya kuumba viumbe.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilio baina yao mnamo siku sita; na wala hayakutugusa machofu. [38]
[38] Ninaapa: Hakika tumeziumba mbingu na ardhi na viumbe viliomo baina yao katika siku sita. Na hatukupata kuchoka. Rejea mambo yaliyo khusu maana ya neno "Siku" za uumbaji katika maelezo ya kitaalamu juu ya Aya za idadi 9 mpaka 12 katika Sura ya "Fuss'ilat". 41:9-12
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa hakika tuliumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina ya hivyo viwili miongoni mwa viumbe kwa muda wa Siku sita, na hatukupata tabu yoyote wala shida. Katika uwezo huu mkubwa kuna dalili ya wazi kuwa Yeye, Aliyetakasika, Ana uwezo wa kuhuisha wafu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net