Qaaf 50:36
قوَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّن قَرْنٍ هُمْ أَشَدُّ مِنْهُم بَطْشًا فَنَقَّبُوا۟ فِى ٱلْبِلَـٰدِ هَلْ مِن مَّحِيصٍ
Na kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao, waliokuwa na nguvu zaidi kuliko hawa! Nao walitanga tanga katika nchi nyingi. Je, walipata pa kukimbilia?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao walio kuwa na nguvu zaidi kuliko hawa! Nao walitanga tanga katika nchi nyingi. Je! Walipata pa kukimbilia? [36]
[36] Na wengi tumekwisha wateketeza kabla ya hawa wanao kadhibisha katika mataifa yaliyo kwisha pita. Wao walikuwa na nguvu na madaraka zaidi kuliko hawa. Wakaizunguka miji wakishughulika kuchungua na kutafuta. Je! Walipata pa kukimbilia wasiangamizwe?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tuliwaangamiza, kabla ya hao (washirikina wa kikureishi), ummah wengi. Walikuwa na nguvu na ujabari kuliko wao. Walizunguka mijini wakafuata kila njia kutaka kuyakimbia maangamivu. Basi je, kuna pakukimbilia popote pakujiepusha na adhabu ya Allah Mtukufu itakapowajia?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net