Qaaf 50:34
قٱدْخُلُوهَا بِسَلَـٰمٍ ۖ ذَٰلِكَ يَوْمُ ٱلْخُلُودِ
(Ataambiwa) ingieni humo kwa salama. Hiyo ndiyo siku ya kudumu daima dawamu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
(Ataambiwa) ingieni kwa salama. Hiyo ndiyo siku ya daima dawamu. [34]
[34] Itasemwa kwa hishima yao: Ingieni Peponi kwa amani. Hiyo siku mtakapo ingia Peponi ndiyo siku ya kubakia milele isiyo na mwisho.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hapo waambiwe hao Waumini, «Ingieni Peponi kuingia ambako ndani yake kuna kusalimika na maafa na shari, na kuna kuhifadhiwa na mambo yote mnayoyachukia. Hiyo ndiyo Siku ya starehe za milele zisizokatika».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net