Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 50 · Aya ya 30

Qaaf 50:30

ق

يَوْمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ ٱمْتَلَأْتِ وَتَقُولُ هَلْ مِن مَّزِيدٍ

Maana

Siku tutakapoiambia Jahanamu: 'Je, umejaa?' Nayo itasema: 'Je, kuna ziada?'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Siku tutapo iambia Jahannamu: Je! Umejaa? Nayo itasema: Je! Kuna ziada? [30]

[30] Siku tutapo iambia Jahannamu kwa kuwatia kiwewe makafiri: Je! Umejaa? Nayo Jahannamu iseme kwa kuwaghadhibikia: Wapo wengine zaidi wa kuwaongeza katika hawa wenye kudhulumu?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakumbushe watu wako, (ewe Mtume), kuhusu siku tutakayoiambia Jahanamu, «Je umeshajaa?» Na Jahanamu iseme, «Je kuna nyongeza yoyote ya majini na binadamu?» Hapo Mola, uliotukuka utukufu wake, Aweke unyayo Wake ndani yake, na hapo ijikusanye na ijikunjekunje na iseme, «Basi! Basi!»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Qaaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net