Qaaf 50:3
قأَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا ۖ ذَٰلِكَ رَجْعٌۢ بَعِيدٌ
Ati tukifa na tukawa udongo...? Kurejea huko kuko mbali!'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ati tukifa na tukawa udongo? Kurejea huko kuko mbali! [3]
[3] Ati baada ya kwisha kufa na tukawa udongo, tutafufuliwa tena? Huko kufufuliwa baada ya kufa ni marejeo yaliyo mbali, hayawi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hivi tutakapokufa tukawa mchanga, itawezekana kurejea baada ya hapo tukawa kama tulivyokuwa? Hayo ni marajeo ambayo kutokea kwake kuko mbali.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net