Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 50 · Aya ya 28

Qaaf 50:28

ق

قَالَ لَا تَخْتَصِمُوا۟ لَدَىَّ وَقَدْ قَدَّمْتُ إِلَيْكُم بِٱلْوَعِيدِ

Maana

(Mwenyezi Mungu) aseme: 'Msigombane mbele yangu. Tayari niliwaletea mbele onyo langu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

(Mwenyezi Mungu) aseme: Msigombane mbele yangu. Nilikuleteeni mbele onyo langu. [28]

[28] Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia makafiri na wenzi wao: Msigombane mbele yangu hapa pahala pa hisabu na malipo. Na Mimi nilikuleteeni mbele duniani onyo juu ya kukufuru kwenu kuukataa Ujumbe wangu niliyo utuma kwenu. Nanyi hamkuamini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Aseme, «msibishane mbele yangu leo kwenye Kisimamo cha Malipo na Hesabu. Kwani hilo halina faida, na mimi niliwaletea duniani onyo la adhabu kwa aliyenikufuru na kuniasi».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Qaaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net