Qaaf 50:20
قوَنُفِخَ فِى ٱلصُّورِ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمُ ٱلْوَعِيدِ
Na litapulizwa baragumu. Hiyo ndiyo Siku ya Miadi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na litapulizwa baragumu. Hiyo ndiyo Siku ya Miadi. [20]
[20] Na baragumu litapulizwa kwa mpulizo wa kuwafufua watu. Kupulizwa huko kutakuwa siku hiyo ya kuteremka adhabu waliyo ahidiwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hapo baragumu litakapopulizwa mpulizo wa pili wa Ufufuzi. mpulizo huo utakuwa kwenye Siku ya kutekeleza adhabu ambayo Allah Mtukufu Aliwaahidi wakanushaji.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net