Qaaf 50:11
قرِّزْقًا لِّلْعِبَادِ ۖ وَأَحْيَيْنَا بِهِۦ بَلْدَةً مَّيْتًا ۚ كَذَٰلِكَ ٱلْخُرُوجُ
Ili iwe ni riziki kwa waja wangu. Na tukaifufua kwa maji nchi iliyokuwa imekufa. Kama hivyo ndivyo utakavyokuwa ufufuaji.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ili iwe ni riziki kwa waja wangu. Na tukaifufua kwa maji nchi iliyo kuwa imekufa. Kama hivyo ndivyo utakavyo kuwa ufufuaji. [11]
[11] Tumeotesha hiyo ili iwe ni riziki kwa waja wetu, na tukaihuisha kwa maji ardhi iliyo kauka mimea yake. Hali kadhaalika ndivyo kufufuliwa wafu kutoka makaburini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Tumeviotesha hivyo viwe ni riziki za waja za wao kuzila kulingana na mahitaji yao, na tukahuisha, kwa maji haya tuliyoyateremsha, ardhi iliyokuwa kavu na kame, haina nafaka wala mimea mingine. Na kama tunavyohuisha, kwa maji hayo, ardhi iliyokufa, tutawatoa nyinyi Siku ya Kiyama mkiwa hai baada ya kufa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net