Qaaf 50:1
ققٓ ۚ وَٱلْقُرْءَانِ ٱلْمَجِيدِ
Qaaf.[1] Ninaapa kwa Qur-ani tukufu!
[1] Herufi hii "Qaaf" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Qaaf. Naapa kwa Qur'ani tukufu! [1]
[1] Qaaf. Hii ni harufi katika harufi za alifbete iliyo fungulia Sura hii kama ilivyo ada ya Qur'ani katika kufungulia Sura kadhaa wa kadhaa kwa harufi kama hii, ili kuwakabili makafiri kama wanaweza kuleta mfano wake, na pia kuwazindua watu wasikilize yanayo somwa. Ninaapa kwa Qur'ani yenye ubora, na utukufu, na hishima kwamba hakika Sisi tumekutuma wewe, ewe Muhammad, ili uwaonye watu kwa hii.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Qāf» Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa mwanzoni mwa sura ya Al-Baqarah. Anaapa Allah Mtukufu kwa Qur’ani tukufu, yenye ubora na heshima.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net