Al-Maaida 5:4
المائدةيَسْـَٔلُونَكَ مَاذَآ أُحِلَّ لَهُمْ ۖ قُلْ أُحِلَّ لَكُمُ ٱلطَّيِّبَـٰتُ ۙ وَمَا عَلَّمْتُم مِّنَ ٱلْجَوَارِحِ مُكَلِّبِينَ تُعَلِّمُونَهُنَّ مِمَّا عَلَّمَكُمُ ٱللَّهُ ۖ فَكُلُوا۟ مِمَّآ أَمْسَكْنَ عَلَيْكُمْ وَٱذْكُرُوا۟ ٱسْمَ ٱللَّهِ عَلَيْهِ ۖ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلْحِسَابِ
Wanakuuliza ni nini wamehalalishiwa? Sema: Mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri na mlichowafundisha wanyama kukiwinda. Mnawafundisha alivyokufunzeni Mwenyezi Mungu. Basi kuleni katika kile walichowakamatia, na mkisomee jina la Mwenyezi Mungu. Na mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanakuuliza wamehalalishiwa nini? Sema: Mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri na mlicho wafundisha wanyama kukiwinda. Mnawafundisha alivyo kufunzeni Mwenyezi Mungu. Basi kuleni walicho kukamatieni, na mkisomee jina la Mwenyezi Mungu. Na mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu. [4]
[4] Ewe Mtume! Waumini wanakuuliza nini walicho halalishiwa katika vyakula na vyenginevyo? Waambie: Mwenyezi Mungu amekuhalalishieni kila chema kipendacho nafsi njema. Na pia amekuhalalishieni kula kinacho windwa na wanyama wenu mlio wafunza kuwinda, kwa kutokana na alivyo kufunzeni Mwenyezi Mungu. Basi kuleni wanacho winda wanyama hao mlio watuma, na mtaje jina la Mwenyezi Mungu pale mnapo watomeza. Na mcheni Mwenyezi Mungu kwa kuzishika sharia zake, wala msikiuke mipaka yake. Tahadharini kumkhalifu Mwenyezi Mungu katika hayo, kwani Yeye ni Mwepesi wa kuhisabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanakuuliza Maswahaba wako, ewe Nabii, «Ni kipi walichohalalishiwa kukila?» Waambie, «Mumehalalishiwa kula vilivyo vizuri na viwindwa vya wanyama mliowafundisha kati ya wanyama wanaowinda kwa kutumia makucha na meno yao, miongoni mwa mbwa, chui na kozi na kama hao kati ya wale wanaofundishwa. Mnawafundisha kuwatafutia viwindwa kwa yale Allah Mtukufu Aliyowafundisha. Basi kuleni wanyama waliowashikia na mlitaje jina la Allah Mtukufu wakati mnapowatuma kuwawindia. Na muogopeni Allah Mtukufu katika yale Aliyowaamrisha na yale Aliyowakataza.» Hakika Allah Mtukufu ni Mwepesi wa kuhesabu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net