Al-Fath 48:17
الفتحلَّيْسَ عَلَى ٱلْأَعْمَىٰ حَرَجٌ وَلَا عَلَى ٱلْأَعْرَجِ حَرَجٌ وَلَا عَلَى ٱلْمَرِيضِ حَرَجٌ ۗ وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ يُدْخِلْهُ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ ۖ وَمَن يَتَوَلَّ يُعَذِّبْهُ عَذَابًا أَلِيمًا
Kipofu hana lawama, wala kiguru hana lawama, wala mgonjwa hana lawama. Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, atamuingiza katika Mabustani ya mbinguni yapitayo mito chini yake. Na atakayegeuka upande, atamuadhibu kwa adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kipofu hana lawama, wala kiguru hana lawama, wala mgonjwa hana lawama. Na mwenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, atamuingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Na atakaye geuka upande atamuadhibu kwa adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yule aliye kipofu kati yenu, enyi watu, hana dhambi, wala aliye kiwete hana dhambi, wala aliye mgonjwa hana dhambi, wanapobaki wasishiriki katika kupigana jihadi pamoja na Waumini, kwa kuwa wao hawawezi. Na Mwenye kumtii Allah Mtukufu na Mtume Wake, Atamtia kwenye mabustani ya Pepo ambayo chini ya miti yake na majumba yake ya fahari itakuwa ikipita mito. Na Mwenye kumuasi Allah Mtukufu na Mtume Wake akabaki ili kukwepa kupigana jihadi pamoja na Waumini, Atamuadhibu adhabu yenye uchungu na kuumiza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net