Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 48 · Aya ya 15

Al-Fath 48:15

الفتح

سَيَقُولُ ٱلْمُخَلَّفُونَ إِذَا ٱنطَلَقْتُمْ إِلَىٰ مَغَانِمَ لِتَأْخُذُوهَا ذَرُونَا نَتَّبِعْكُمْ ۖ يُرِيدُونَ أَن يُبَدِّلُوا۟ كَلَـٰمَ ٱللَّهِ ۚ قُل لَّن تَتَّبِعُونَا كَذَٰلِكُمْ قَالَ ٱللَّهُ مِن قَبْلُ ۖ فَسَيَقُولُونَ بَلْ تَحْسُدُونَنَا ۚ بَلْ كَانُوا۟ لَا يَفْقَهُونَ إِلَّا قَلِيلًا

Maana

Wale waliobaki nyuma watasema: 'Mtakapokwenda kuchukua ngawira, tuacheni tukufuateni!' Wanataka kuyabadili maneno ya Mwenyezi Mungu. Sema: 'Hamtatufuata kabisa. Mwenyezi Mungu alikwisha sema hivi zamani.' Hapo watasema: 'Bali nyinyi mnatuhusudu.' Sivyo, bali walikuwa hawafahamu ila kidogo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Walio baki nyuma watasema: Mtapo kwenda kuchukua ngawira, tuacheni tukufuateni! Wanataka kuyabadili maneno ya Mwenyezi Mungu. Sema: Hamtatufuata kabisa. Mwenyezi Mungu alikwisha sema kama hivi zamani. Hapo watasema: Bali nyinyi mnatuhusudu. Siyo, bali walikuwa hawafahamu ila kidogo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Watasema wale walioachwa nyuma utakapoondoka, wewe na Maswahaba wako kuelekea kwenye ngawira za (Khaybar) ambazo Allah Mtukufu Aliwaahidi nyinyi kuwa mtazipata, «Tuacheni tuende na nyinyi huko (Khaybar)!» wakiwa wanataka kwa hilo kubadilisha ahadi ya Allah Mtukufu kwenu. Waambie, «Hamtatoka pamoja na sisi kwenda Khaybar, kwa kuwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, alituambia kabla hatujarudi Madina kwamba ngawira za (Khaybar) ni za wale waliohudhuria (Hudaybiyah) pamoja na sisi.» Watasema, «Mambo sivyo kama mnavyosema. Allah Mtukufu Hakuwaamrisha nyinyi hili. Nyinyi mnatukataza kwa uhasidi wenu tusije tukapata ngawira pamoja na nyinyi.» Mambo sivyo kama walivyodai, bali wao walikuwa hawaelewi amri za Allah Mtukufu kuhusu haki zao na wajibu wao wa kidini isipokuwa kidogo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Fath

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net