Muhammad 47:7
محمديَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِن تَنصُرُوا۟ ٱللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ
Enyi mlioamini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu, naye atakunusuruni na ataiimarisha miguu yenu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu. [7]
[7] Enyi mlio amini! Mkiinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu, na Yeye atakunusuruni muwashinde maadui zenu, na ayatilie nguvu mambo yenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo, mkiinusuru Dini ya Allah Mtukufu kwa kupigana jihadi katika njia Yake na kuhukumu kwa Kitabu Chake na kufuata amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake, Allah Mtukufu Atawapa ushindi juu ya maadui zenu na Atazithibitisha nyayo zenu wakati wa kupigana.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net