Muhammad 47:32
محمدإِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَصَدُّوا۟ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَشَآقُّوا۟ ٱلرَّسُولَ مِنۢ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ ٱلْهُدَىٰ لَن يَضُرُّوا۟ ٱللَّهَ شَيْـًٔا وَسَيُحْبِطُ أَعْمَـٰلَهُمْ
Kwa hakika wale waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu na wakapingana na Mtume baada ya uongofu kwisha wabainikia, hao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote. Naye ataviangusha vitendo vyao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa hakika walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu na wakapinzana na Mtume baada ya kwisha wabainikia uwongofu, hao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote. Naye ataviangusha vitendo vyao. [32]
[32] Hakika walio kufuru na wakazuia njia ya Mwenyezi Mungu, na wakenda kinyume na Mtume kwa inda na ukaidi, baada ya kwisha wadhihirikia uwongofu, hao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote. Na Yeye atayabat'ilisha yote waliyo yatenda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale waliokataa kuwa Menyezi Mungu Ndiye Mola wa haki Peke Yake Asiye na mshirika, wakawazuia watu na Dini Yake, wakaenda kinyume na Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na wakampiga vita baada ya wao kujiwa na hoja na alama za kuwa yeye ni Nabii kutoka kwa Allah Mtukufu, hawataidhuru Dini ya Allah Mtukufu kitu chochote, na atayatengua malipo ya matendo yao waliyoyafanya duniani, kwa kuwa wao hawakutaka kwa matendo hayo radhi za Allah Mtukufu Aliyetukuka.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net