Muhammad 47:30
محمدوَلَوْ نَشَآءُ لَأَرَيْنَـٰكَهُمْ فَلَعَرَفْتَهُم بِسِيمَـٰهُمْ ۚ وَلَتَعْرِفَنَّهُمْ فِى لَحْنِ ٱلْقَوْلِ ۚ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ أَعْمَـٰلَكُمْ
Na tungelipenda, tungelikuonyesha hao na ungeliwatambua kwa alama zao. Lakini bila ya shaka utawajua kwa namna ya msemo wao. Na Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyenu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tungeli penda tungeli kuonyesha hao na ungeli watambua kwa alama zao; lakini bila ya shaka utawajua kwa namna ya msemo wao. Na Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyenu. [30]
[30] Tungeli penda bila ya shaka tungeli kuonyesha hao wanaafiki, nawe ungeli wajua kwa alama zao, na ungeli wajua kwa namna yao wanavyo sema. Na Mwenyezi Mungu anajua ukweli wa vitendo vyenu vyote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau tungetaka, ewe Nabii, tungekuonyesha hao watu wenyewe, ukawatambua kwa alama zilizo wazi kwao. Na kwa hakika utawajua kutokana na maneno yao yaliyodhihirika yenye kuonyesha malengo yao. Na kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, hakuna chochote kinachofichika cha matendo ya wanaomtii na matendo ya wanaomuasi, na Atamlipa kila mmoja kwa anachostahili.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net