Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 47 · Aya ya 28

Muhammad 47:28

محمد

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ ٱتَّبَعُوا۟ مَآ أَسْخَطَ ٱللَّهَ وَكَرِهُوا۟ رِضْوَٰنَهُۥ فَأَحْبَطَ أَعْمَـٰلَهُمْ

Maana

Hayo ni kwa sababu wao waliyafuata yale yaliyomchukiza Mwenyezi Mungu na wakachukia yanayomridhisha, basi akaviangusha vitendo vyao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hayo ni kwa sababu wao waliyafuata yaliyo mchukiza Mwenyezi Mungu na wakachukia yanayo mridhisha, basi akaviangusha vitendo vyao. [28]

[28] Kufishwa namna hiyo ya kutisha katika hali hiyo ni kwa kuwa hakika wao waliufuata upotovu ulio mkasirisha Mwenyezi Mungu, na wakaichukia Haki inayo mpendeza Mwenyezi Mungu. Basi akayabat'ilisha waliyo yatenda.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Adhabu hiyo waliyostahili na wakaipata ni kwa kuwa waliyafuata mambo yanayomfanya Allah Mtukufu Awakasirikie ya kumtii Shetani, na wakayachukia yale yanayomfanya Awe radhi nao ya matendo mema, na miongoni mwayo ni kupigana na wakanushaji, baada ya kulifanya hilo ni lazima juu yao, ndipo Allah Mtukufu Akazibatilisha thawabu za matendo yao, miongoni mwa sadaka, kuunga udugu na yasiyokuwa hayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Muhammad

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net