Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 46 · Aya ya 21

Al-Ahqaf 46:21

الأحقاف

وَٱذْكُرْ أَخَا عَادٍ إِذْ أَنذَرَ قَوْمَهُۥ بِٱلْأَحْقَافِ وَقَدْ خَلَتِ ٱلنُّذُرُ مِنۢ بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِۦٓ أَلَّا تَعْبُدُوٓا۟ إِلَّا ٱللَّهَ إِنِّىٓ أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ

Maana

Na mtaje ndugu wa kina 'Adi, alipowaonya watu wake kwenye vilima vya mchanga. Na kwa yakini waonyaji wengi walitokea kabla yake na baada yake kuwaambia: 'Msimuabudu isipokuwa Mwenyezi Mungu. Hakika mimi nawahofia ije kukupateni adhabu ya siku iliyo kuu.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mtaje ndugu wa kina A'di, alipo waonya watu wake kwenye vilima vya mchanga. Na kwa yakini waonyaji wengi walitokea kabla yake na baada yake kuwaambia: Msimuabudu isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Hakika mimi nakukhofieni isikupateni adhabu ya siku iliyo kuu. [21]

[21] Mtaje Hud, mwenzao kabila ya A'di, alipo wahadharisha watu wake wanao kaa Ah'qaaf, kwenye vilima vya mchanga. Na Mitume kadhaa walikuja kabla yake na baada yake kwa maonyo kama yake ya kusema: Msimuabudu ila Mwenyezi Mungu. Mimi nakukhofieni isikupateni adhabu yenye vitisho vikuu. Maskani ya kabila hii ilikuwa huko Ah'qaaf, kwenye vilima vya mchanga. Na wapi hapo Ah'qaaf? Zipo khitilafu. Baadhi ya wanazuoni wa taarikh (historia) wanasema kuwa hapo ni baina ya Yaman na Oman mpaka Hadhramaut na Shihr, yaani mashariki ya kusini ya Bara Arabu. Na baadhi ya wachunguzi wa zama za karibu wanaona ni mashariki ya A'qaba, wakitegemea maandishi ya Nabat'ia waliyo yakuta katika magofu ya hekalu walilo livumbua katika mlima wa Arim. Walikuta pembezoni mwa mlima huo mabaki ya siku za Jahiliya za zamani. Wakasahihisha kuwa hapo ndipo ilipo Arim iliyo tajwa katika Qur'ani tukufu. Kisha kabila hiyo ikatoka hapo kabla ya Uislamu, na hapana kilicho baki chao isipo kuwa chemchem ya maji ambayo wafanyi biashara na watu wa misafara wakishukia hapo katika njia yao kwendea Shamu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka, ewe Mtume, Nabii wa Allah Mtukufu Hūd, ndugu yao kina ‛Ᾱd kinasaba na siyo kidini, alipowaonya watu wake kuwa watashukiwa na adhabu ya Allah Mtukufu wakiwa kwenye nyumba zao hapo Aḥqāf (mahali kwenye mchanga mwingi) kusini mwa Arabuni. Na kwa hakika wamepita Mitume wakawaonya watu wao kabla ya Hūd na baada yake wakiwaambia, «Msimshirikishe Allah Mtukufu na kitu chochote mnapomuabudu. Mimi nawachelea nyinyi adhabu ya Allah Mtukufu katika Siku yenye kitisho kikubwa, nayo ni Siku ya Kiyama».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahqaf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net