Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 45 · Aya ya 30

Al-Jaathiya 45:30

الجاثية

فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ فَيُدْخِلُهُمْ رَبُّهُمْ فِى رَحْمَتِهِۦ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْمُبِينُ

Maana

Ama walioamini na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawatia katika rehema yake. Huko ndiko kufuzu kuliko wazi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ama walio amini na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawatia katika rehema yake. Huko ndiko kufuzu kulio wazi. [30]

[30] Basi ama walio amini na wakatenda vitendo vyema, Mola wao Mlezi atawatia katika Pepo yake. Malipo hayo ndio kufuzu kulio bainika, kulio wazi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ama wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake duniani, wakafuata amri Zake na wakajiepusha na makatazo Yake, hao Atawatia Mola wao kwenye Pepo Yake kwa rehema Zake. Kuingia huko ndiko kufaulu kuliko wazi ambako hakuna kufaulu kupita huko.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Jaathiya

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net