Ad-Dukhaan 44:56
الدخانلَا يَذُوقُونَ فِيهَا ٱلْمَوْتَ إِلَّا ٱلْمَوْتَةَ ٱلْأُولَىٰ ۖ وَوَقَىٰهُمْ عَذَابَ ٱلْجَحِيمِ
Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda kutokana na adhabu ya Jahannamu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu, [56]
[56] Huko Peponi hawataonja mauti baada ya mauti ya kwanza waliyo kwisha yaonja duniani ulipo kwisha muda wao wa kuishi, na Mola wao Mlezi atawalinda na adhabu ya Motoni.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawataonja kifo, wachamungu hao, huko Peponi, baada ya kifo cha kwanza walichokionja duniani. Na Allah Mtukufu Atawakinga, hao wachamungu,na adhabu ya moto wa Jaḥīm, kwa wema Wake na hisani itokayo Kwake, Aliyetakasika na kuwa juu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net