Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 44 · Aya ya 49

Ad-Dukhaan 44:49

الدخان

ذُقْ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْكَرِيمُ

Maana

Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu! [49]

[49] Ataambiwa kwa kejeli na maskhara: Onja hii adhabu kali, kwani ati wewe si ndiye mtukufu mwenye nguvu katika kaumu yako, ndiye mheshimiwa unavyo jiona mwenyewe!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ataambiwa mfanya dhambi huyo mbaya, «Onja adhabu hii unayoadhibiwa kwayo Leo! Hakika wewe ni mheshimiwa katika watu wako, ulio mtukufu kwao.» Katika haya kuna kumfanyia maskhara na kumlaumu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ad-Dukhaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net