Ad-Dukhaan 44:39
الدخانمَا خَلَقْنَـٰهُمَآ إِلَّا بِٱلْحَقِّ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui. [39]
[39] Hatukuziumba hizo ila kwa umbo lilio ambatana na hikima, kwa nidhamu iliyo thibiti yenye kuonyesha ushahidi wa kuwepo Mwenyezi Mungu wa pekee, Mwenye uwezo. Lakini wengi wa hawa wameghafilika, wamo katika upofu, hawazioni dalili hizi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hatukuviumba hivyo viwili isipokuwa kwa haki ambayo ndiyo mpango wa Allah Mtukufu katika kuumba Kwake na kupelekesha mambo Kwake. Lakini wengi wa hawa washirikina hawalijui hilo, na kwa hivyo hawavitii akilini vitu viwili hivyo, kwa kuwa wao hawatarajii kupata malipo mema wala hawaogopi mateso.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net